Mchakato wa uchaguzi wa kuziba nafasi zilizowazi ndani ya Yanga unaendelea ambapo uongozi wa klabu hiyo umetangaza majina ya Wajumbe walioteuliwa kuunda kamati ya uchaguzi.
Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Yanga Siza Lyimo amesema wanatarajia kuanza mchakato wa uchaguzi mara baada ya kuwapa taarifa Wajumbe hao.
"Mwanzoni tulikuwa na kamati ambayo ilionekana ina mapungufu"
"Lakini baada ya sisi viongozi kukutana, tulikubaliana na wenzetu kamati ya uchaguzi ya TFF, Baraza na Michezo na Mkurugenzi wa Michezo kwa kushirikiana na Waziri ili kupata Kamati mpya itakayoungana na wenzetu wa TFF ili kufanya utaratibu wa uchaguzi na mchakato kwenda kwa wakati."
"Aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ni Venance Mwamoto (Mbunge), Katibu wake ni Seif Gulamali (Mbunge wa Igunga) na wajumbe wengine wawili."
Awali uchaguzi wa Yanga ulipangwa kufanyika Januari 13 2019 lakini haukufanyika kufuatia baadhi ya Mwanachama kwenda Mahakamani kuweka zuio.
Hata hivyo tofauti iliyojitokeza awali baina ya Yanga na TFF inaonekana kuwa imemalizwa na sasa mchakato huo wa uchaguzi utaendelea kwa kushirikisha pande zote mbili