Vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga leo wanashuka dimba la Majaliwa huko Ruangwa kuikabili Namungo Fc kwenye mchezo wa kombe la FA (ASFC) hatua ya 16 bora
Yanga ilitua Ruangwa juzi ikiwa na kikosi cha wachezaji 20 ambapo kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera alisema wamejiandaa kikamilifu kushinda nchezo huo
Timu itakayoibuka na ushindi katika mchezo wa leo itatinga robo fainali
"Tumejiandaa vizuri. Nafahamu mchezo huu ni wa mtoano, tukipigwa tunatolewa kwenye mashindano"
"Tunahitaji kushinda ili tuweze kuingia hatua inayofuata. Lengo letu ni kutwaa ubingwa," amesema Zahera
Licha ya kuwa ugenini, Yanga inatarajia kupata uungwaji mkono wa mashabiki wengi kwani juzi wakati ilipowasili Ruangwa, mji huo ulizizima kwa shangwe za mashabiki wa timu hiyo