Licha ya mashabiki kumpongeza kwa kucheza vizuri katika mchezo wa juzi dhidi ya Namungo Fc, mlinda lango wa Yanga Klaus Kindoki amesema bado hajafikia ubora wake na atazidi kujiimarisha zaidi
Juzi Kindoki aliibuka nyota wa mchezo baada yakuisaidia Yanga kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Azam (ASFC) kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namungo Fc mkoani Lindi
"Watu wanaona nimecheza vizuri inawezekana, lakini mimi binafsi bado nahitaji kuonyesha uwezo zaidi ili niisaidie timu yangu," Kindoki amenukuliwa na Mwanaspoti
"Watu wanaponipongeza wananipa morali ya kujituma zaidi na sio kubweteka, kwasasa jambo linalonisaidia sasa tunawasiliana vyema na wachezaji wenzangu wakati nafika lugha ya kiswahili ilinisumbua."
Kindoki aliyetua Yanga kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akiletwa na Kocha Mwinyi Zahera, hakuanza vizuri maisha yake katika klabu ya Yanga lakini kiwango chake sasa kinaonekana kuimarika