Pluijm ajivunia uanachama wa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Mar 2019
Pluijm ajivunia uanachama wa Yanga

Hakuna ubishi Yanga ndio iliyompa ujiko Kocha Hans Pluijm na kumtambulisha kwa mashabiki wa soka nchini ilipoingia naye karandarasi ya kuinoa Januari 2014, kitu hicho kumbe bado kipo akilini mwa Mholanzi huyo na kudai haiwezi kuitosa jumla klabu hiyo.

Pluijm alisema licha ya kujivunia mafanikio aliyoyapata Yanga, lakini anaendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa klabu hiyo na ataendelea kuwasiliana nayo kokote alipo baada ya kutemana na Azam FC.

Yanga iliachana na Pluijm msimu wa 2017/18 kumchukua Mzambia, George Lwandamina kisha akaenda zake Singida United na baadaye msimu huu Azam kwa mkataba wa mwaka mmoja uliositishwa na mabosi wa klabu hiyo.

“Kuondoka Tanzania haimaanishi ndio mwisho wa uhusiano wangu na Yanga, nimetokea kuipenda kutoka moyoni sio tu kwa sababu niliifundisha bali imenipa heshima kubwa nilichukua kadi kwa kumanisha na sio mihemko.

"Kubwa zaidi nitaendelea kuwa na mawasiliano ya karibu sana na yule ambaye ndiye alifanikisha kutua Yanga mara ya kwanza lakini mashabiki ambao waliniunga mkono katika kazi zangu, ipo kichwani na moyoni haitafutika.”

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
9h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
12h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
17h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
21h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’