Zahera kuleta wachezaji sita wa kigeni

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Mar 2019
Zahera kuleta wachezaji sita wa kigeni

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema tayari ana majina ya wachezaji sita wa kigeni ambao anakusudia kuwasajili kwa ajili ya kukiimarisha kikosi cha Yanga msimu ujao

Akizungumza kwenye Mkutano wa viongozi wa Matawi ya klabu ya Yanga ambao  yeye alialikwa, Zahera amesema mipango hiyo itafanikiwa kama Wana Yanga watachangia fedha za kutosha

"Watu wahamasishane kuhusu kuichangia Yanga SC, nimepanga kuisuka klabu hii msimu ujao ambapo nitaleta wachezaji 6 wageni wazuri kwa gharama ndogo kuzidi hata wazawa," amesema Zahera

Katika Mkutano huo ambao ulifanyika leo Alhamisi Makao Makuu ya klabu ya Yanga, viongozi wa matawi waliafikiana kuendeleza ushawishi kwa wanachama ili wajitoe kuichangia timu kuweza kufikia malengo

Katika kutambua mchango wake kwa klabu ya Yanga, Zahera atatunukiwa kadi ya heshima ya uanachama wa Yanga

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
5h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’