Ten aitaka Simba imkemee Manara

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Mar 2019
Ten aitaka Simba imkemee Manara

Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema uongozi wa Simba utahusika kama kuna jambo lolote baya litamtokea kocha Mwinyi Zahera kutokana na kauli za uchochezi zilizotolewa na msemaji wa Simba Haji Manara

Manara jana alitoa kauli za uchochezi dhidi ya kocha Zahera wakati akihojiwa na redio mbalimbali kuzungumzia mchezo wa ligi ya mabingwa kati ya Simba dhidi ya AS Vita Club utakaopigwa leo katika dimba la Taifa

"Kauli za kichochezi dhidi ya kocha Zahera Mwinyi, wana Yanga wote tuamini kuwa jambo lolote baya litakalo mpata kocha wetu basi Uongozi wa Simba unahusika," amesema Ten

"Kama sivyo, viongozi wa Simba wajitokeze hadharani kukanusha au kuzikemea kauli hizo"

"Soka ni mchezo wa kiungwana, vipi wengine waugeuze kuwa sehemu ya uchochezi na ubaguzi?"

Pichani juu ni wakati Rayon Sports ilipokuja kucheza na Yanga mchezo wa kombe la Shirikisho ambapo kiungo Haruna Niyonzima na aliyekuwa kocha msaidizi wa Simba Masudi Djuma walifika katika hotel ya timu hiyo kusalimiana na ndugu zao kutoka Rwanda

Jana Manara alidai kitendo cha Zahera kwenda kuwasalimia AS Vita Club ni cha hujuma!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’