Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya kuhamasisha uchangiaji wa Yanga, Mh Anthony Mavunde ameyataka Matawi ya klabu ya Yanga kote nchini kuiga Matawi ya Dodoma na Mbeya ambayo tayari yamefikia na kuvuka malengo ya uchangishaji wa fedha
Akizungumza na Yanga TV, Mavunde amesema walikubaliana kila tawi la Yanga kukusanya angalau Tsh Milioni moja ili kuweza kupata Tsh Bil 1.5
Amesema Tawi la Yanga Mbeya limevuka malengo hayo baada ya kuwa limekusanya Tsh Mil 2 huku likijiwekea malengo ya kukusanya Mil 10
Tawi la Makao Makuu Dodoma nalo tayari limekusanya Mil 1 fedha hizo zikipatikana punde tu baada ya tawi hilo kufunguliwa
Aidha Mavunde amewataka Wanayanga waendelee kuichangia timu ili kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa
Kocha Mwinyi Zahera ametaka kuanza mapema zoezi la usajili hivyo amesisitiza ni muhimu fedha zikapatikana kabla ligi haijamalizika