Tambwe, Makambo, Ngasa wanolewa kuibeba Yanga dhidi ya Alliance FC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Mar 2019
Tambwe, Makambo, Ngasa wanolewa kuibeba Yanga dhidi ya Alliance FC

Mwishoni mwa wiki hii Yanga inakabiliwa na mchezo muhimu wa robo fainali kombe la Azam (ASFC) dhidi ya Alliance Fc utakaopigwa March 30 kwenye uwanja wa CCM Kirumba

Kocha Msaidizi wa Yanga Noel Mwandila amesema ni lazima wajiandae kikamilifu kuhakikisha wanapata matokeo yatakayo-wapeleka hatua ya nusu fainali

Kocha huyo anayekaimu nafasi ya Zahera, amesema wanaufahamu ubora wa Alliance Fc, kupitia michezo miwili ambayo wamekutana nao kwenye ligi, wanafahamu nini wafanye ili waweze kupata matokeo

"Hatuna cha kupoteza kuelekea mchezo huo tupo makini kila idara tunapambana kuhakikisha tunapata matokeo uwanja wa Kirumba, sio kazi rahisi kwetu kwani tunakutana na wapinzani ambao ni bora kila idara," Mwadila amenukuliwa na Mwanaspoti

"Wana nguvu, wachezaji vijana na wana kasi tunatarajia kukutana na changamoto kubwa kutoka kwao lakini tumejipanga kukabiliana nazo kwasababu tunatambua umuhimu wa mchezo huo, Ngassa na Makambo wanakasi ya kukimbia na mipira Tambwe atakaa tayari kwaajili ya kumalizia mipira mirefu itakayokuwa inapigwa"

Mwandila ameongeza kuwa hawawezi kucheza mchezo sawa na wapinzani wao wanatarajia kutumia mbinu mbadala ambayo itawasaidia wao kupata matokeo kama ilivyokuwa michezo iliyopita na kuweka wazi kuwa lengo lao ni kupata matokeo mapema ili kuwatoa mchezoni wapinzani wao.

Yanga imekutana mara mbili na Alliance Fc katika michezo ya ligi na Yanga kushinda yote

Kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa Yanga ilishinda mabao 3-0 kabla ya kushinda 1-0 katika mchezo wa marudiano uliopigwa dimba la CCM Kirumba

Itarejea mkoani Mwanza tena katika uwanja wa CCM Kirumba dhidi ya vijana hao machachari kuwania tiketi muhimu ya kutinga nusu fainali kombe la FA (ASFC)

Baada ya mchezo huo, Yanga itaendelea kutumia dimba la CCM Kirumba kwa michezo yake yote ya nyumbani wakati uwanja wa Taifa utakapokuwa umefungwa kupisha michuano ya kombe la AFCON ya vijana

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’