Yanga imebakiza michezo saba kumaliza msimu lakini beki wake kisiki Kelvin Yondani huenda akakosa nusu ya michezo hiyo baada ya jana kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar
Yondani alitolewa nje kwenye dakika ya 82 baada ya kumpiga kiwiko mchezaji wa Kagera Sugar
Kulingana na kanuni za uendeshaji wa ligi kuu ya Tanzania Bara msimu huu, Yondani atakosa michezo mitatu inayofuata
Mchezo wa kwanza atakaokosa ni dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa April 17 2019 kisha kufuatiwa na mchezo dhidi ya Azam Fc utakaopigwa April 29 2019
Pengine pia atakosa mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Lipuli Fc ambao ratiba ya awali inaonyesha utafanyika mwanzoni mwa mwezi wa tano
Katika michezo hiyo Yanga itawategemea walinzi Andrew Vicent Chikupe, Abdallah Shaibu 'Ninja' na Said Juma ambaye amefanya vizuri katika michezo aliyopata nafasi wakati Chikupe alipokuwa majeruhi na Ninja akiwa anatumikia adhabu