Kadi za njano zimeendelea kumkosesha michezo muhimu kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' ambaye hatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachoikabili Mtibwa Sugar keshokutwa mkoani Morogoro
Fei Toto amefikisha kadi tatu za njano hivyo kukosa sifa ya kucheza mchezo huo wa mzunguuko wa 32 ligi kuu ya Tanzania Bara
Huo utakuwa mchezo wa nne kwa Fei Toto msimu huu anakosa kutokana na wingi wa kadi za njano
Licha ya kukosekana kwa Fei Toto, kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema hana wasiwasi kuelekea mchezo huo kwani wapo wachezaji wanaoweza kucheza nafasi yake
Kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar Yanga pia itamkosa beki wake kisiki Kelvin Yondani anayetumikia adhabu ya kukosa michezo mitatu baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar
Zahera amesema wanahitaji kushinda michezo yote saba iliyobaki ili kuwa na nafasi ya kuwania ubingwa wa ligi kuu