Nahodha Msaidizi wa Yanga Juma Abdul anakabiliwa na changamoto ya kupata namba mbele ya 'dogo' Paulo Godfrey 'Boxer' ambaye tangu apandishwe kikosi cha kwanza kutoka Yanga B, kiwango chake kimekuwa kikipanda siku hadi siku
Abdul ambaye pia amekuwa akikabiliwa na majeraha ya mara kwa mara, amepewa program maalum na kocha Mwinyi Zahera itakayomsaidia kupunguza uzito na kumrejesha katika ubora wake
Baada ya mchezo dhidi ya African Lyon ambao Abdul alicheza, Zahera alikiri kuwa beki huyo bado hana mpinzani katika nafasi anayocheza lakini kwa sasa anakabiliwa na changamoto ya kuwa mzito
Zahera alimtaka Abdul ambaye ni mtaalum wa kupiga krosi, afanyie kazi mwili wake ili kurejesha kasi aliyokuwa nayo misimu miwili iliyopita
Zahera anaamini Abdul bado ana nafasi katika kikosi cha Yanga lakini kwanza ni lazima apunguze mwili