Uchaguzi utaleta Yanga mpya - Mkwasa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Apr 2019
Uchaguzi utaleta Yanga mpya - Mkwasa

Wakati wanachama wa Yanga wakisalia na siku 16 kabla ya kufanya uchaguzi wa nafasi mbalimbali, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema uchaguzi huo utaiondoa klabu kwenye mtikisiko wa uchumi.

Mkwasa alisema, Yanga iliyumba kutokana na kutokuwa na viongozi kwa muda mrefu ambao wangeweza kuweka mipango kwaajili ya maendeleo ya timu yao.

"Wakati naingia Yanga kama Katibu Mkuu, nilifanya kazi na Mwenyekiti (Yusuf Manji) kwa siku tano tu akawa ameingia kwenye matatizo"

"Tumekaa muda mrefu bila mwenyekiti, tulipambana, hadi pale tulipofikia," alisema Mkwasa.

Alisema klabu hiyo ambayo inapitia katika mtikisiko wa uchumi, itakapokuwa na uongozi kila kitu kitakwenda sawa.

Yanga itafanya uchaguzi Mei 5 jijini Dar es Salaam kuchagua mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe wa kamati ya utendaji ambao walijiuzuru kwa nyakati tofauti.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
19m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’