Haya ndio yanayoibua mashaka ya 'kubebana'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Apr 2019
Haya ndio yanayoibua mashaka ya 'kubebana'

April 17 michezo ya ligi ilipangwa kuchezwa saa nane mchana sababu ikitajwa michuano ya AFCON U17 hasa kwa kuwa Serengeti Boyz ilikuwa ikishuka dimbani saa kumi jioni kuchuana na Uganda

Hata hivyo leo licha ya Serengeti Boyz kushuka dimbani saa kumi jioni kuchuana na Angola, Bodi ya ligi imebadili muda wa mchezo kati ya Kagera Sugar dhidi ya Simba kutoka saa nane na kuwa saa kumi kamili jioni

Kimsingi, mapema kabla ya michezo ya juzi wadau walilalamikia uamuzi wa TFF wa kubadili muda wa michezo kwa kisingizo cha AFCON U17 lakini maoni yao yalipuuzwa

Lakini leo kwa kuwa ni Simba peke yake inayoshuka dimbani wameona ni vyema kubadili muda wa mchezo huo

Naamini kama ingekuwa ni timu nyingine ambayo ilipaswa kucheza saa nane, muda huo usingebadilishwa

Uamuzi huu ni wa hovyo kwa kuwa unadhihirisha upendeleo wa TFF kwa baadhi ya timu.

Kuna timu nyingi tu msimu huu zilipangiwa kucheza saa nane na michezo ikafanyika lakini huu wa Simba kwa nini ubadilishwe muda saa chache kabla ya mchezo?

Huu ni upendeleo wa dhahiri, na hakika hali hii inadhihirisha kwa nini Simba mpaka leo imeshuka dimbani mara 23 tu huku ligi ikipaswa kumalizika katika kipindi cha wiki nne

Hii ni aibu kwa soka la Tanzania, tusijidanganye, hatuwezi kusonga mbele kwa utaratibu huu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
19m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’