Ligi Kuu ya Wanawake maarufu kama Serengeti Lite inaendelea leo ambapo mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Princess dhidi ya Simba Queens utapigwa kwenye uwanja wa Karume
Mchezo huo utakuwa wa kisasi kwa akina dada wa Yanga Princess ambao wana kumbukumbu ya kubugizwa mabao 7-0 katika mchezo wa duru ya kwanza uliopigwa katika uwanja huo
Katika msimamo wa ligi hiyo Yanga Princess wanashika nafasi ya saba wakiwa wamejikusanyia alama 19 wakati wapinzani wao Simba Queens wanashika nafasi ya nne wakiwa wamejikusanyia alama 31
ADVERTISE HERE