Yanga yajitathmini faini za kila mara

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Apr 2019
Yanga yajitathmini faini za kila mara

Uongozi wa Yanga umesema utachukua hatua ili 'kujisahihisha' kuepuka faini za Shirikisho la Soka nchini (TFF) kutokana na matukio yanayohusisha imani za kishirikina yanayojiri kwenye baadhi ya michezo yake

Matukio ya kutotumia mlango rasmi wa kuingia uwanjani yameigharimu sana Yanga msimu huu ambapo jana ilipigwa faini ya nne baada ya kufanya kosa hilo mkoani Mtwara ilipokwenda kucheza na Ndanda Fc

Yanga tayari imepigwa faini zilizoigharimu timu hiyo zaidi ya Tsh Milioni 10 kutokana na matukio hayo ya kuingia uwanjani kwa kutumia 'njia za panya'

Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema matukio hayo yanachangiwa zaidi ya Wananchi ambao kimsingi ndio wenye timu na wanahusishwa kuisimamia timu inapokwenda kucheza

"Umefika wakati sasa tunapaswa kuwaelimisha watu wetu wafahamu athari tunazopata kutokana na kuendekeza imani hizi," amesema

"Lazima ifahamike kila mchezo una kanuni na taratibu zake. Tukiendelea kuvunja kanuni kutokana na imani zetu, tutaendelea kuigharimu timu"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’