Kuna taarifa kuwa wachezaji wa Yanga leo waligoma kufanya mazoezi ya asubuhi wakishinikiza walipwe mishahara ya miezi mitatu pamoja na malimbikizo ya fedha za usajili
Kulingana na taarifa iliyoripotiwa na mtandao wa Mwanaspoti mapema leo, wachezaji walikataa kufanya mazoezi wakiwatuhumu viongozi wa Yanga kuwa 'wamewapuuza'
Tulimtafuta msemaji wa Yanga Dismas Ten bila ya mafanikio ili atoe ufafanuzi wa sintofahamu hiyo
Hata hivyo suala la madai ya wachezaji ni la muda mrefu ambapo Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omary Kaya aliwahi kusema kuwa watamaliza madai hayo kwa awamu
Kwa sasa Yanga inaongozwa na Kamati Maalum baada ya viongozi wote kujiuzulu kupisha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika May 05 2019
ADVERTISE HERE