Kumekuwa na utata kuhusu timu ambayo May 23 itachuana na Sevilla katika mchezo wa kirafiki utakaoihusisha Yanga au Simba
Klabu ya Sevilla tayari imethibitisha ujio wake May 23 huku TFF ikiwa bao haijaweka wazi kati ya Yanga au Simba ni timu ipi ambayo itacheza nao
Inadaiwa pendekezo la awali lilikuwa kwa timu za Yanga na Simba kuunda kikosi kimoja. Hata hivyo pendekezo hilo lilikataliwa na timu zote
Kuna uwezekano mkubwa TFF ikaandaa mchezo kati ya Yanga na Simba ili mshindi wa mchezo huo achuane na Sevilla
Kampuni ya SportPesa imefanikisha ujio wa Sevilla inayoshiriki ligi kuu ya Hispania La Liga
Kampuni hiyo inayodhamini vilabu vya Yanga na Simba, pia ni mmoja wa wadhamini wa La Liga
Β
ADVERTISE HERE