Zahera aanika mbinu alizotumia kuimaliza Azam Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Apr 2019
Zahera aanika mbinu alizotumia kuimaliza Azam Fc

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema ulikuwa ni mpango wake wa mchezo kuwaachia mpira Azam Fc huku wao wakitumia mashambulizi ya kushtukiza

Zahera amesema kama wachezaji wake wangekuwa makini wangeweza kushinda mabao sio chini ya manne

"Tulifahamu ubora wa wapinzani wetu, hivyo tuliandaa mpango maalum wa kuweza kuwadhibiti," amesema

"Tulikubaliana wote tujilinde tunapokuwa hatuna mpira na tushambulie kwa kasi tunapopata mpira"

"Mbinu yetu ilifanikiwa kwani tulitengeneza nafasi nyingi za kufunga kuliko Azam ambao walikuwa na mpira kwa muda mrefu"

Aidha akizungumzia mbio za ubingwa, Zahera amesema hatma ya ubingwa haiko mikononi mwa Yanga kutokana na matukio ya waamuzi

"Kuna mechi tano waamuzi wametunyima ushindi waziwazi. Kama ligi ya Tanzania ingekuwa inaendeshwa vizuri pengine leo tungekuwa tayari tumetwaa ubingwa," amesema

"Lakini nafurahi kuona TFF wameanza kuchukua hatua baada ya juzi kuwafungia waamuzi waliochezesha mchezo wa KMC dhidi ya Simba"

"Pengine baada ya uamuzi huo, waamuzi wengine hawatafanya makosa"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’