Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti kwenye uchaguzi wa Yanga utakaofanyika keshokutwa Jumapili, Elias Mwanjala ametangaza kujitoa katika kinyan'ganyiro hicho
Mwanjala amesema amelazimika kujitoa kutokana na kukabiliwa na majukumu mengine
Aidha Mwanjala ni mjumbe kamati ya utendaji TFF na ni Mwenyekiti wa Katiba na sheria, amesema anaweza kuisaidia Yanga kupitia nafasi hiyo
Kujitoa kwake kunafanya wagombea watatu wabaki katika kinyan'ganyiro cha kuwania Uwenyekiti wa Yanga ambao ni Dk Mbette Mshindo Msolla, Dr Jonas Tiboroha na Baraka Igangula
Uchaguzi utafanyika keshokutwa Jumapili, May 05 ukumbi wa bwalo la Polisi, Osterbay jijini Dar es salaam
ADVERTISE HERE