Moja ya ahadi alizotoa Mwenyekiti mpya wa Yanga Dk Mbette Mshindo Msolla ni kumpatia kocha Mwinyi Zahera fedha zote za usajili alizotaka
Zahera alihitaji kupatiwa angalau Tsh Bilioni 1.5 kwa ajili ya kukamilisha usajili wa wachezaji wapya
Dk Msolla amesema Zahera atapatiwa fedha hizo na hata akitaka zaidi ataongezwa
"Fedha zote alizotaka kocha Zahera kwa ajili ya usajili tutampatia. Hata kama akitaka tumuongeze, tutafanya hivyo"
"Lakini kikubwa zaidi ni kuwa fedha hizo atapatiwa yeye mwenyewe. Hatutaki kutumia watu wa kati maana wamekuwa wakiongeza gharama ili kujinufaisha," alisema
Jana baada ya uchaguzi kukamilika, Msolla na viongozi wapya waliochaguliwa walikutana kuweka mikakati kwenda wa kuipa sapoti Yanga inayocheza na Lipuli Fc leo mkoani Iringa