Idadi ya mechi kuamua hatma ya wachezaji Yanga

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
13 May 2019
Idadi ya mechi kuamua hatma ya wachezaji Yanga

Michakato ya usajili tayari imeanza kushika kasi ambapo dirisha la usajili litafunguliwa rasmi mwezi ujao na kufungwa mwishoni mwa mwezi wa saba

Macho na masikio ya Wanayanga wengi yameelekezwa kwa uongozi mpya wa timu hiyo na kocha Mwinyi Zahera kwani kimsingi, ni wao waliobeba matumaini yao wakiwa na shauku ya kuona timu inarejesha makali yake ya miaka kadhaa iliyopita

Huu ni msimu wa pili Wanayanga hawana furaha ya kweli kwani timu yao haina ushindani ukilinganisha na watani zao Simba ambao wanatambia mafanikio wanayopata sasa

Licha ya kupita kwenye hali ngumu ya kiuchumi, juhudi zimefanyika na zinaendelea kufanyika kwa wadau wa Yanga kuichangia timu yao ili iweze kuunda kikosi imara

Matumaini ni makubwa, ambapo uongozi mpya wa Yanga umeahidi kuirejesha furaha ya Wana Jangwani msimu ujao

Ili kuhakikisha timu yake inakuwa imara msimu ujao, Zahera ameweka vigezo kwa wachezaji wanaopaswa kuendelea kuichezea Yanga

Mcongomani huyo amepanga kutumia idadi ya michezo aliyocheza kila mchezaji kama kigezo cha kuwaengua baadhi yao

Inaelezwa wachezaji wote ambao hawakufanikiwa kucheza angalau nusu ya mechi za msimu huu hawataendelea kuichezea Yanga msimu ujao

Aidha Zahera ameweka sifa kwa wachezaji wapya kuwa ni lazima wawe na uwezo mkubwa kuliko wachezaji waliopo

Zahera amepanga kusajili wachezaji wa kikosi cha kwanza na sio wa kukaa benchi.

Ametaka wachezaji wapya wawe chachu ya kuwafanya wachezaji waliopo kujituma zaidi ili kupata nafasi ya kucheza jambo ambalo anaamini litaongeza ushindani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’