Zahera ataja sababu ya Ngasa kukosekana mchezo dhidi ya Ruvu Shooting

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 May 2019
Zahera ataja sababu ya Ngasa kukosekana mchezo dhidi ya Ruvu Shooting

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema winga Mrisho Ngasa hakuweza kucheza jana mchezo dhidi ya Ruvu Shooting baada ya kuugua ghafla

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo, Zahera alisema Daktari wa timu Dk Bavu alishauri mchezaji huyo asitumike kwenye mchezo huo hivyo kuamua kumtumia Paulo Godfrey 'Boxer' wingi ya kulia

"Ngasa alipata matatizo muda mfupi baada ya kuwa tumepata kifungua kinywa. Alianza kutapika mfululizo na baada ya kupatiwa huduma na Daktari wa timu Dk Bavu, alishauri asicheze," alisema Zahera

Akizungumzia mchezo huo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0, Zahera aliwapongeza wachezaji wake kwa ushindi huo huku akifichua hawakuwa wamefanya mazoezi tangu walipocheza na Biashara United May 10

"Tulipata changamoto ya usafiri kutoka Mwanza hali iliyopelekea tuchelewe kurudi jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo. Hata baada ya kurudi tulilazimika kuwapa wachezaji mapumziko kwani walikuwa wamechoka"

"Nilifahamu mchezo wa leo (jana) hautakuwa mwepesi kwetu, lakini nimefurahi tumeweza kutumia moja ya nafasi tulizotengeneza ingawa tulikuwa na uwezo wa kufunga mabao zaidi kwenye kipindi cha kwanza"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’