Zahera aenda Benin kusaka mbadala wa Makambo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 May 2019
Zahera aenda Benin kusaka mbadala wa Makambo

Baada ya kusambaa kwa taarifa za mshambuliaji wa Yanga Heritier Makambo kusajiliwa na Horoya AC ya Guinea kwa mkataba wa miaka mitatu, Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla alifafanua kuwa dili hilo limeihusisha klabu yake na Makambo aliondoka nchini na Kocha Mwinyi Zahera

Hata hivyo imefahamika Zahera alilekea nchini Bennin ambako amekwenda kufanya mazungumzo na mshambuliaji mwingine

Halitakuwa jambo la kushangaza kama mshambuliaji huyo atakuwa Marcellin Koukpo ambaye alikuja msimu uliopita lakini usajili wake kukwamishwa na wajanja wachache waliokuwa wakitaka 'ten percent'

Koukpo mshambuliaji wa Kimataifa wa Benin, alikaa nchini kwa zaidi ya wiki mbili kabla ya kuamua kuondoka baada ya kupishana na viongozi wa Yanga

Mshambuliaji huyo alipendekezwa na aliyekuwa kocha wa Yanga msimu uliopita, George Lwandamina na alifanyiwa majaribio na kocha Mwinyi Zahera kabla ya kuibuliwa taarifa za 'uzushi' kuwa ameshindwa majaribio

cut

Baada ya kumuuza Makambo, Yanga inaweza kusajili washambuliaji wawili ambapo mmoja anaweza kuwa huyo Mbenin huku timu hiyo ikihusishwa na mshambuliaji wa Gor Mahia Jacques Tuyisenge na Roderick Matuma raia wa Zimbabwe anayekipiga kunako klabu ya Fc Lupopo

Dirisha la usajili litafunguliwa mwezi ujao ambapo uongozi wa Yanga umepania kukiimarisha kikosi chake wakijipanga kutumia kati ya Bil 1.5 hadi Bil 2

Hata hivyo Yanga imedhamiria kukamilisha masuala ya usajili mapema hasa ikizingatiwa Zahera ndiye msimamizi Mkuu wa mchakato huo

Mwanzoni mwa mwezi wa sita Zahera atarejea kwao Congo kwa ajili ya majukumu ya timu ya Taifa kuelekea fainali za AFCON zitakazofanyika Misri kuanzia Juni 21 2019

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’