Makambo awashukuru mashabiki Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 May 2019
Makambo awashukuru mashabiki Yanga

Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Heritier Makambo amewashukuru mashabiki wa timu kwa sapoti waliyompa katika kipindi cha mwaka mmoja aliotumikia klabu hiyo

Makambo yuko katika hatua za mwisho kukamilisha uhamisho wa kwenda klabu ya Horoya AC, mabingwa wa ligi kuu ya Guinea

"Nitawakumbuka mashabiki wa Yanga kwa upendo na sapoti yao kwangu. Watabaki moyoni kwangu," ameandika Makambo kwenye mtandao wa kijamii

Mshambuliaji huyo aliyetua Yanga kutoka FC Lupopo kwa mkataba wa miaka miwili, atakuwa ametumikia nusu ya mkataba wake hivyo kuinufaisha Yanga katika mauzo yake

Mkurugenzi wa ufundi wa Horoya AC anatarajiwa kuja Tanzania wiki ijayo kuonana na uongozi wa Yanga ili kukamilisha dili la mshambuliaji huyo

Licha ya kuwa tayari amesaini mkataba wa awali kuitumikia Horoya AC, Makambo hataweza kuichezea Horoya kabla ya mabosi wa timu hiyo kumalizana na Yanga ili kupata cheti cha uhamisho wa Kimataifa(ITC)

cut

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla alisema Makambo alizivutia timu nyingi, pia wanayo barua kutoka Ubelgiji ambako kuna timu inahitaji huduma mshambuliaji huyo kinara wa kufunga mabao ya vichwa

Katika mechi 42 alizocheza Yanga, Makambo amefunga mabao 21 na kutoa pasi mbili za mabao

Ameondoka akiwa kinara wa upachikaji mabao kwenye kikosi cha Yanga, akiwa amefunga mabao 16 ligi kuu ya Tanzania Bara

Hakuna uhakika kama atarudi nchini kumalizia michezo miwili ya ligi iliyobaki

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’