Yanga yaipania Mbeya City

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 May 2019
Yanga yaipania Mbeya City

Licha ya kuwa na nafasi finyu ya kutwaa ubingwa msimu huu, Yanga imepania kumaliza ligi kwa kishindo kesho ikiikaribisha Mbeya City katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Uhuru

Vijana wa Mwinyi Zahera wamekuwa wakijifua uwanja wa chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam

Habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni kuwa watapata fursa ya kumuaga mshambuliaji wao Heritier Makambo anaelekea kuondoka baada ya ligi kumalizika

Licha ya kusaini mkataba wa awali klabu ya Horoya AC, Makambo bado ni mchezaji halali wa Yanga mpaka hapo viongozi wa Horoya watakapokuja jijini Dar es salaam kumalizana na Yanga

Inaelezwa Yanga ina ofa nyingine tatu zinazomuhusu mshambuliaji huyo aliyetua mwanzoni mwa msimu akitokea FC Lupopo

cut

Makambo ameifungia Yanga mabao 16 kwenye ligi msimu huu, atakuwa na nafasi ya kuongeza idadi hiyo ya mabao katika michezo miwili iliyobaki

Yanga itakamilisha msimu kwa kuivaa Azam Fc May 28 katika mchezo mwingine wa 'kukata na shoka' utakaopigwa uwanja wa Uhuru

Msimu uliopita Yanga ilipoteza mchezo wa mwisho dhidi ya Azam Fc kwa kufungwa mabao 3-1.

Viongozi wa Yanga wamepania kuhakikisha timu inamaliza msimu bila ya kufungwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
58m ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
4h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
9h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
13h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’