Bodi ya Ligi kupitia Mtendaji wake Boniface Wambura inatarajiwa kutoa ufafanuzi wa timu zilizoshuka daraja baada ya ligi kuu ya Tanzania Bara kukamilika jana

Kumekuwa na sintofahamu juu ya timu ipi inapaswa kuungana na African Lyon kushuka daraja kati ya Stand United na Kagera Sugar
Kulingana na takwimu zilizotolewa na Bodi ya Ligi hapo jana, Stand United na Kagera Sugar zote zina alama 44 huku pia zikiwa na tofauti sawa ya mabao -11
Ilielezwa sheria ya 'head-head' ilitumika kuishusha daraja Kagera Sugar
Baada ya TFF kutoa msimamo wa mwisho wa ligi, Kagera Sugar iliweka hadharani matokeo yote iliyopata msimu mzima ambapo matokeo hayo yanaifanya timu hiyo iwe na alama 44 na tofauti ya mabao -11 lakini kwa Stand United takwimu zinaonyesha timu hiyo ina tofauti ya mabao -12
Matokeo hayo yamedhihirishwa na msimamo wa mwisho wa ligi uliotolewa na Azam TV ambao unazishusha daraja Stand United na African Lyon