Tutashinda hata kwenye uwanja mbovu - Nsajigwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Sep 2017
Tutashinda hata kwenye uwanja mbovu - Nsajigwa
Kocha Msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa amesema licha ya uwanja wa Majimaji kutokuwa mzuri, timu yake itapambana kuhakikisha inapata ushindi kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom utakaopigwa kesho, Septemba 16.

Akihojiwa na Yanga TV, Nsajigwa amesema hali ya uwanja wa Majimaji hairidhishi lakini hilo haliwezi kuwakwamisha kuondoka na alama zote tatu.

Amesema ili kuwa bingwa lazima timu iwe na uwezo wa kupata ushindi inapocheza kwenye viwanja vyenye changamoto kama Majimaji.

"kucheza Kwenye viwanja vya aina hizi ndiyo tabia mojawapo ya kuwa bingwa,tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunashinda mchezo wa kesho," amesema Nsajigwa.

Naye nahodha Nadir Haroub Cannavaro ameunga mkono maneno ya Nsajigwa lakini pia amesisitiza Yanga imejipanga kuondoka na alama zote tatu.

Mchezo wa Majimaji dhidi ya Yanga umekuwa gumzo kwenye viunga vya mji wa Songea. Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkali.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’