Umri ni moja ya vigezo vinavyotumiwa na kocha Mwinyi Zahera kusajili wachezaji wapya kwenye kikosi chake
Zahera ameonekana kupendelea zaidi wachezaji vijana ambao ndio anaowasajili katika mchakato unaoendelea
Miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa, ni beki Lamine Moro pekee mwenye umri wa miaka 25, wengi wana umri kati ya miaka 20 na 23
Licha ya wachezaji hao kuwa na umri mdogo, lakini wengi tayari wana uzoefu wa soka la Kimataifa
Asilimia kubwa ya wachezaji wanaosajiliwa na Yanga, wanazichezea/wamezichezea timu za Taifa
Faida kubwa mbili ambazo Yanga inaweza kuzipata kutokana na wachezaji hao ni kwanza inaweza kuwatumia kwa muda mrefu
Lakini pili wanakuwa na thamani kubwa katika soko la usajili
cutMpira wa sasa ni biashara na Yanga imejipanga kunufaika katika biashara hiyo ya kuuza wachezaji
Inaelezwa kocha Zahera ametaka wastani wa umri wa kikosi chake uwe chini ya miaka 25
Hata hivyo Yanga imekuwa na utamaduni wa kukuza vipaji vya wachezaji vijana
Hata kikosi chake cha msimu uliopita, wachezaji ambao umri wao ulikuwa zaidi ya miaka 25 hawazidi sita