Zahera akata mzizi wa fitina usajili wa Ajib

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Jun 2019
Zahera akata mzizi wa fitina usajili wa Ajib

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amedai kushangazwa na taarifa anazozisikia kuwa viongozi wa Yanga wanafanya majadiliano ya kumpa mkataba mpya nahodha wa timu hiyo Ibrahim Ajib

Zahera amesema alishamuondoa Ajib kwenye mipango yake baada ya mchezaji huyo kutakiwa kujiunga na TP Mazembe

Zahera ambaye yuko Hispania katika majukumu ya timu ya Taifa ya DR Congo inayojiandaa na fainali za AFCON 2019, amesema taarifa za uwepo wa majadiliano hayo hazifahamu

"Baada ya TP Mazembe kumtaka na mwenyewe kukubali kujiunga nao, nilimuondoa katika mipango ya kikosi changu cha msimu ujao," amesema

"Ripoti niliyowaachia viongozi inabainisha wachezaji wote tunaowahitaji kwa ajili ya msimu ujao, Ajib hayumo"

Hivi karibuni Ajib alikana taarifa zinazodai kuwa alishasaini mkataba wa awali na klabu ya Simba, kinachosubiriwa ni mkataba wake na Yanga kumalizika Juni 30 ili atambulishwe

"Sijasaini Simba wala Yanga ingawa yapo mazungumzo yanaendelea. Yakikamilika kila kitu kitawekwa hadharani naweza kucheza timu yoyote hata Yanga kama tutakubaliana"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’