Jumamosi tutaandika Historia - Mutta

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Jun 2019
Jumamosi tutaandika Historia - Mutta

Katibu wa Kamati ya Hamasa na Uchangishaji Yanga Deo Mutta amesema Kamati hiyo inahitimisha kazi yake kwa kuandika Historia siku ya Jumamosi Juni 15 2019 katika tukio la Harambee ya KUBWA KULIKO litakalofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam

Akizungumza na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya klabu ya Yanga Jangwani jijini Dar es salaam, Mutta amesema tukio hilo la Jumamosi ni mwendelezo wa matukio ya kuichangia Yanga yaliyozinduliwa mkoani Dodoma April 06 2019

Amesema mkoani Dodoma walizindua kampeni ambayo lengo lake lilikuwa kuhakikisha mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani inaweza kushiriki katika kuichangia Yanga

Amesema zoezi hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa

Tukio la Diamond Jubilee litakamilisha kazi ya kamati yao iliyoundwa maalum kufanikisha upatikanaji wa fedha kuiwezesha Yanga kuboresha kikosi chake

Mutta amesema maandalizi kuelekea tukio hilo litakaloanza saa nne asubuhi mpaka saa 10 jioni yamekamilika kwa asilimia 90

Wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wamealikwa kwenye tukio hilo Kubwa Kuliko

cut

Miongoni mwa wageni walioalikwa ni Wazee waliotengeneza Historia katika klabu ya Yanga, Wachezaji waliowahi kucheza Yanga, Wasanii mbalimbali (muziki na bongomuvi), Wanachama wa Yanga, wapenzi na mashabiki wa timu hiyo

Amesema Jumamosi Yanga itaandika historia ambayo itabaki kwenye vitabu vya kumbukumbu kwa miaka mingi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’