Winga Deus Kaseke ni miongoni mwa wachezaji ambao wamemaliza mikataba kunako klabu ya Yanga na mpaka sasa bado hakuna mazungumzo juu ya mkataba mpya
Kaseke aliyerejea Yanga kutoka Singida United msimu uliomalizika, amesema kwa sasa ni mchezaji huru na anakaribisha kwa mazungumzo timu zinazohitaji huduma yake
Kaseke alirejeshwa Yanga msimu uliopita ili kuongeza nguvu kwenye kikosi cha timu hiyo kilichoshiriki michuano ya kombe la Shirikisho
Hata hivyo baadae alishindwa kujihakikishia namba kwenye kikosi cha Mwinyi Zahera
Ikiwa tayari imesajili mawinga wawili, Patrick Sibomana na Issa Birigimana, Yanga pia inahusishwa kumuwania kiungo mshambuliaji wa K Sharks Duke Abuya
Zahera ameweka mkazo kusajili mawinga wenye kasi ambao watakwenda sambamba na falsafa yake ya mpira wa kushambulia kwa kasi