Mashabiki wa Yanga na wadau mbalimbali wa soka nchini wameipongeza Yanga kwa kufanikisha usajili wa kiungo Mapinduzi Balama aliyeitumikia Alliance Fc msimu uliopita
Balama alitambulishwa na Yanga jana baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria
Msimu uliomalizika, Balama alikuwa 'injini' ya kutengeneza mashambulizi ya kikosi cha alliance akishirikiana vyema na washambuliaji Blaise Bigirimana na Dickson Ambundo
Usajili wa Balama unatajwa kuwa usajlili bora ambao umefanywa na Yanga kwa wachezaji wa ndani mpaka sasa
Anaungana na Abdulaziz Makame na Ally Ally kuwa wachezaji watatu wa ndani ambao tayari usajili wao Yanga umethibitishwa
ADVERTISE HERE