Dili la Ulimwengu kutua Yanga lapotelea hewani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Jul 2019
Dili la Ulimwengu kutua Yanga lapotelea hewani

Klau ya Yanga, imeachana na mpango wa kumsainisha mkataba mshambuliaji Thomas Ulimwengu, kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Awali, klabu hiyo ilikuwa na nia ya kumsainisha straika huyo anayecheza JS Soura ya Algeria na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo, ilieleza kuwa tayari wanao washambuliaji watatu ambao wana uwezo mzuri hivyo wameona haina haja ya kumsainisha.

"Tulikuwa tunamuhitaji Ulimwengu, lakini hata hivyo tumeona kiwango chake hakitofautiani na wachezaji wengine ambao tunao, hivyo tumeamua kuachana naye kwenye mipango yetu," kilieleza chanzo hicho

Alisema kwa sasa wamekamilisha usajili kwa wachezaji wote ambao walikuwa wanahitajiwa na kocha hivyo kilichobaki kwa sasa ni kujiandaa kwa kambi inayotarajia kuanza Julai 7 kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu pamoja na michuano ya kimataifa.

Alisema wanaamini kwa usajili waliofanya utaisaidia timu hiyo kutimiza malengo ambayo wamejiwekea, ikiwa pamoja na kutwaa ubingwa wa ligi kuu, ambao kwa sasa umechukuliwa na wapinzani wao Simba kwa misimu miwili mfululizo.

Bingwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’