Kukosekana kwa beki kisiki Kelvin Yondani jana mchezo dhidi ya Algeria kuliiathiri safu ya ulinzi ya Stars kwa kiasi fulani na kukubali kuchapwa mabao 3-0
Hata hivyo akicheza mchezo wake wa kwanza kwenye michuano0 ya Afcon, beki mpya wa Yanga Ally Mtoni 'Sonso' alionyesha ukomavu wa hali ya juu kwenye mchezo huo
Sonso alipewa majukumu ya Yondani ambaye alikuwa majeruhi
Pamoja na kukosa uzoefu wa mashindano ya kimataifa haikuwa tatizo kwake, Sonso alicheza kwa kujiamini kama ambavyo ameichezea Lipuli Fc msimu uliopita
Sonso ni moja ya usajili bora uliofanywa na Yanga kwenye safu ya ulinzi
Ujio wake Jangwani, pamoja na mabeki wengine, wataifanya Yanga isiwe timu rahisi kufungika msimu ujao
ADVERTISE HERE