Kesho Jumamosi Yanga inashuka uwanja wa Uhuru kucheza mchezo wa mzunguuko wa nne ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Ndanda FC.
Yanga itashuka dimbani ikiwa na azma moja tu, kuondoka na alama zote tatu.
Ushindi ni lazima kwa Yanga kwa kuwa itakuwa inacheza kwenye uwanja wake wa nyumbani. Lakini pia inahitaji alama tatu iweze kuifikia Simba yenye alama nane na kuweka hai matumaini yake ya kutetea ubingwa.
Kikosi cha Yanga hakina majeruhi wapya zaidi ya Amissi Tambwe na Benno Kakolanya ambao wameanza mazoezi mepesi.
Kocha George Lwandamina huenda akatumia kikosi kilekile cha mchezo uliopita dhidi ya Majimaji na mabadiliko pekee akafanya kwenye namba ya Kamusoko ambapo katika mchezo huo Raphael Daudi alicheza kutokana na nahodha huyo msaidizi kuwa majeruhi.
Kamusoko amepona majeraha yake na yuko tayari kurejea dimbani.
Wachezaji Obrey Chirwa na Geofrey Mwashiuya huenda wakendelea kutumika kama washambuliaji wa kutokea pembeni huku Ajib na Ngoma wakiendelea kuwa washambuliaji wa kati.
Hakutarajiwi kuwa na mabadiliko kwenye safu ya ulinzi ambapo mlindalango Youthe Rostand, Juma Abdul, Gadiel Michael, Andrew Vicent, Kelvin Yondani na kiungo mkabaji Papi Kabamba Tshishimbi wameweza kumshawishi mwalimu Lwandamina kuwaanzisha kwenye kikosi cha kwanza.

ADVERTISE HERE