Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla anafanya ziara ya kutembelea matawi ya klabu ya Yanga mikoani
Akiwa mkoani Mtwara jana Dk Msolla aliitaka TFF kuivunja Kamati ya Waamuzi na kuunda nyingine kwani msimu uliopita Kamati hiyo ilionyesha madhaifu makubwa
Dk Msolla alisema baadhi ya waamuzi walikuwa wakichezesha mechi za timu moja tu
"Hili jambo halipendezi kwa hiyo ombi langu ni ile kamati ya uamuzi ya kitaifa wajitazame, ikiwezekana TFF waivunje na waunde mpya, haiwezekani miaka miwili, mitatu kuna malalamiko ya waamuzi na hayapungui," alisema
Dk Msolla alisema kuelekea msimu mpya wa ligi makosa ya waamuzi hayapaswi kujirudia.
Msimu uliopita ulikabiliwa na changamoto nyingi za maamuzi ya 'hovyo' klabu ya Yanga ikiwa miongoni mwa timu zilizoathiriwa zaidi na maamuzi hao