Yanga isake mbadala wa hawa

Admin By Admin
β€’
23 Jun 2017
Yanga isake mbadala wa hawa
Haruna Niyonzima
Huyu uongozi tayari umeshatangaza kuachana nae pale mkataba wake utakapomalizika Julai 21 baada kushindwana nae kwenye dau la usajili.

Viongozi wametumia busara kuokoa zaidi ya Mil 130 zilizokuwa apewe Niyonzima sasa wanaweza kuitumia pesa hiyo kusajili hata wachezaji wawili wenye uwezo wa juu hata zaidi yake.

Donald Ngoma
Huyu ana kila dalili ya kumfuata Niyonzima Simba. Kulingana na taarifa aliyoitoa Mkwassa wiki iliyopita, Ngoma alitakiwa kuwasili Juni 15 kusaini mkataba mpya baada ya ule wa awali kumalizika.

Ngoma ni miongoni mwa wachezaji ambao kocha Lwandamina alipendekeza wapewe mikataba mipya lakini mpaka leo hajarudi na wala hajatoa taarifa yoyote.

Hata hivyo huyu alisumbua sana msimu uliopita, aliisaidia Yanga kwenye mzunguuko wa kwanza tu. Katika mzunguuko wote wa pili hakucheza na pia alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokuwa wakifanya migomo ya mara kwa mara wakati timu ilipokumbwa na ukata.

Huyu aachwe aende tu, timu itafute straika mwingine.

Vicent Bossou
Licha ya kuwa mmoja wa wachezaji tegemeo msimu uliopita, Bossou kama ilivyokuwa kwa Ngoma, alifanya migomo mingi sana pale ukata ulipoikumba Yanga.

Ingawa ilikuwa ni haki yao kudai mishahara lakini migomo hiyo ilipelekea kushusha morali ya wachezaji wengine.

Mkataba wake umemalizika na yuko tayari kusaini mkataba mpya lakini anataka 'pesa ndefu'.

Hakuna haja ya kusumbuana nae, asajiliwe beki mwingine wa kati mzalendo asaidiane na waliopo.

Dida na Barthez
Deogratius Munish 'Dida' mkataba wake umemalizika na kwa kuwa ameitwa kufanya majaribio nchini Afrika Kusini uongozi umemruhusu akafanye majaribio akishindwa ndio arudi kusaini mkataba mpya.

Ali Mustafa 'Barthez' yeye mkataba wake bado una miezi kadhaa umalizike lakini nadhani hayuko kwenye mpiango ya kocha George Lwandamina.

Oscar Joshua
Huyu nae ameitumikia Yanga kwa mafanikio miaka yote minne lakini sasa nadhani aruhusiwe akatafute timu nyingine ili aendelee kulinda kipaji chake.

Naamini viongozi wa Yanga wanafanya kazi usiku na mchana kusuka upya kikosi cha Yanga na haitakuwa ajabu tukishuhudia sura ngeni nyingi msimu ujao.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’