Hatma ya kipa namba moja Yanga mikononi mwa Manyika

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Jul 2019
Hatma ya kipa namba moja Yanga mikononi mwa Manyika

Baada ya msimu uliopita kukumbwa na changamoto eneo la ulinzi wa lango hasa baada ya Kakolanya kugoma, uongozi wa Yanga umesajili magolikipa wanne

Klaus Kindoki na Ramadhani Kabwili wameongezewa nguvu kwa kuletewa walinda lango wa Kimataifa Farouk Shikalo na Metacha Mnata

Mkufunzi mpya wa makipa Peter Manyika atakuwa na kazi ya kuamua nani awe kipa namba moja kulingana na ubora wa makipa hao

Manyika ambaye yuko kambini Morogoro akiwanoa Kindoki, Kabwili na Metacha, amesema kwa sasa hawezi kufahamu yupi anapaswa kuwa kipa namba moja

"Tumesajili makipa wanne, kwa sasa ninao watatu kambini, namsubiri huyo mmoja afike ili niweze kufahamu ubora wake," amesema

Shikalo bado hajatua kambini kwa kuwa alipewa mapumziko kutokana na ushiriki wake katika michuano ya Afcon akiwa na Kenya na kombe la Kagame akiwa na Bandari Fc

Hata hivyo Shikalo ndiye anatabiriwa kuwa huenda akawa mlinda lango namba moja wa mabingwa hao wa kihistoria

Lakini kuwa na makipa wote wenye ubora ni faida kwa klabu kwani wanaweza kupewa nafasi kwa zamu kulingana na mashindano ambayo timu inashiriki

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’