Mapema tu Mganda Juma Balinya ameanza kuteka mioyo ya mashabiki wa Yanga kutokana na makali anayoonyesha
Baada ya Yanga kumuuza aliyekuwa mshambuliaji wake tegemeo Heritier Makambo, baadhi ya mashabiki walipata hofu
Akiwa tayari ameifungia Yanga mabao mawili kwenye michezo ya kirafiki, Balinya ameonyesha huenda akawasahaulisha kabisa mashabiki kuhusu Makambo
Ingawa bado ni mapema sana, lakini Balinya ameanza kujijengea ufalme kwenye kikosi cha Yanga
Wakati Balinya akianza kuonyesha makali, kazi itakuwa kwa washambuliaji wengine Sadney Urikhob aliyetua hivi karibuni na Maybin Kalengo aliyeanza kwa kasi kabla ya kupata majeraha ya kifundo cha mguu
Sadney alichelewa kuripoti kambini, pengine atahitaji muda zaidi ya kujifua
Lakini wengi wana matumaini makubwa kwake kutokana na umahiri wake katika kuzifumania nyavu