Bigirimana haihofii jezi ya Ajib

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Jul 2019
Bigirimana haihofii jezi ya Ajib

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Issa Bigirimana amekabidhiwa jezi namba 10 ambayo ilikuwa ikitumiwa na aliyekuwa nahodha wa timu hiyo Ibrahim Ajib ambaye ametimkia Simba

Ajib ameondoka Yanga akiacha rekodi ya kipekee msimu uliopita, akiibuka kinara wa pasi za mabao, akitoa pasi 17 za mabao huku mwenyewe akifunga mabao saba

Bigirimana amesema mpaka kusajiliwa na Yanga ina maana timu hiyo imejiridhisha na uwezo wake hivyo ataitendea haki jezi hiyo

"Yanga ina timu nzuri ambayo inakupa changamoto kama mchezaji kujituma mwenyewe. Ushindani utakuwa mkubwa, kila mchezaji ni mzuri hapa naamini tutafanya vizuri," amesema

Wakati Bigirimana akibeba jezi namba 10, mshambuliaji Sadney Urikhob amekabidhiwa jezi namba 17 iliyokuwa ikitumiwa na Amissi Tambwe

Juma Balinya chaguo lake lilikuwa jezi namba 18 wakati Maybin Kalengo amekabidhiwa jezi namba 19 iliyokuwa ikitumiwa na Heritier Makambo

Patrick Sibomana amechukua jezi namba 9, Mapinduzi Balama namba 7, Lamime Moro namba 25, Abdulaziz Makame namba 21, Ally Mtoni namba 3, Ally Ally namba 14, Marcelo namba 2 na Mustapha Suleyman yeye amekabidhiwa jezi namba 15

Mlinda lango Farouk Shikalo yeye atavaa jezi namba 1 wakati Metacha Mnata amechukua jezi namba 30

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
9h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
13h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
14h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
14h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’