Mahadhi ataja sababu ya kutoonekana kambini Morogoro

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Jul 2019
Mahadhi ataja sababu ya kutoonekana kambini Morogoro

Winga Juma Mahadhi ni miongoni mwa wachezaji watakaoendelea kukipiga Jangwani baada ya uongozi wa Yanga kumuongeza mkataba

Hata hivyo 'kiberenge' huyo bado hajaonekana uwanjani wakati wenzie wanaendelea kujifua mkoani Morogoro

Msimu mzima uliopita Mahadhi hakupiga kabisa 'gozi la ng'ombe' baada ya kuvunjika mguu kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger

Mahadhi amefichua kuwa sio muda mrefu ataonekana dimbani baada ya kupona majeraha hayo

"Kwa sasa nimepona kwa kiasi kikubwa, wanayanga wawe na subira kidogo siku sio nyingi wataniona uwanjani" amesema

Licha ya kutoonekana uwanjani kwa muda mrefu, kocha Mwinyi Zahera ameonyesha kuwa na imani nae na kupendekeza aongezwe mkataba

Mahadhi alitua Yanga misimu mitatu iliyopita akitokea klabu ya Coastal Union

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
15h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
20h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’