Ratiba CAF kumrejesha Zahera mapema

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jul 2019
Ratiba CAF kumrejesha Zahera mapema

Baada ya ratiba ya michezo ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa kutoka, Yanga inapaswa kutumia vyema wiki mbili zilizobaki kufanya maandalizi kabambe kabla ya kuikabili Township Rollers ambayo imeweka kambi Afrika Kusini

Mabingwa hao wa Botswana wamewahi kuja hapa nchini kucheza na Yanga mwaka jana na kuondoka na ushindi wa mabao 2-1, sio timu ya kubeza

Msimu uliopita Rollers walicheza hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa

Wameanza maandalizi yao mapema pengine wakilenga zaidi michuano ya ligi ya mabingwa ambayo ina 'ukwasi' mkubwa

Julai 27 watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Simba huko Afrika Kusini

Kocha Mwinyi Zahera ambaye taarifa za awali zilibainisha kuwa angewasili Alhamisi ijayo, huenda akatua mapema zaidi

Kocha Msaidizi Noel Mwandila ameisimamia timu tangu ilipotua mkoani Morogoro wiki mbili zilizopita

Hata hivyo program zote za mazoezi zimeandaliwa na Zahera na licha ya kutokuwepo, uongozi wa Yanga umesema Mcongomani huyo amekuwa akiwasiliana kwa karibu na Mwandila ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa

Hata hivyo uwepo wake utaongeza morali ya wachezaji katika maandalizi hayo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’