Zahera asubiriwa Morogoro

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Jul 2019
Zahera asubiriwa Morogoro

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera anatarajiwa kuwasili nchini wakati wowote kuungana na kambi ya kikosi cha Yanga mkoani Morogoro

Zahera alikwenda Ufaransa kwa mapumziko baada ya kumaliza majukumu ya timu ya Taifa ya DR Congo ambayo yeye ni kocha Msaidizi

Mcongomani huyo alimuachia Kocha Msaidizi Noel Mwandila majukumu ya kukiandaa kikosi cha timu hiyo kuelekea msimu mpya

Akizungumza jana baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya ATN Academy, Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh alisema kocha huyo atawasili nchini siku yoyote kuanzia jana

Aidha taarifa za ndani zimebainisha kuwa Mcongomani huyo anatarajiwa kuwasili nchini kesho Alhamisi

Aidha Hafidh alisema licha ya kutokuwepo, Zahera amekuwa akifuatia maandalizi ya timu

Yanga iko mkoani Morogoro ikijiandaa na michezo ya awali kabla ya kuanza ligi mwezi ujao

August 04 itashuka uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa kuhitimisha wiki ya Mwananchi, timu ikayochuana nayo ikitarajiwa kutangazwa leo

Aidha August 10 itaumana na Township Rollers kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa hatua ya awali

Mchezo huo utapigwa uwanja wa taifa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’