Kiingilio Mwananchi Day ni buku tano tu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Jul 2019
Kiingilio Mwananchi Day ni buku tano tu

Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza viingilio katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Kariobangi katika Wiki ya Mwananchi kuwa ni Sh 5000 na VIP 100,000, mechi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Agosti 4 mwaka huu.

Mchezo huo maalumu kwa ajili ya kutambulisha wachezaji wao unatarajiwa kuchezwa saa kumi jioni ambapo utatanguliwa na mechi kati ya Bongo Fleva na Bongo Movi na mavetenali wa Yanga na Pamba.

Akizungumza Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Hamasa wa klabu hiyo, Deo Muta alisema mchezo huo utakuwa katika viingilio vitatu ambapo kiingilio cha chini ni Sh 5,000 kwa mzunguko wa orange.

Muta alisema kwa upande wa VIP B kiingilio kitakuwa Sh 30000 wakati VIP A itakuwa ni Sh 100,000.

"Tunawaomba mashabiki wetu na wadau wa soka kujitokeza kwa wingi kuja kushuhudia usajili bora uliofanywa na klabu yetu ikiwa ni sambamba na burudani kutoka kwa wasanii na wakongwe wa ligi."

"Kutakuwa na wakongwe waliofanya kazi kubwa kipindi hicho Yanga ambao naamini kuwa watu hawawafahamu tutaweka majina kwenye jezi zao watakazovaa wakati wa kucheza ili kuondoa tabu kwa mashabiki kushindwa kutambua nani anamiliki mpira," alisema Muta.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’