Uongozi wa Yanga umesema August 04 itakuwa siku ya kihistoria kwa Wanayanga kwani ni siku ambayo furaha itarejea rasmi baada ya kikosi cha timu hiyo kutambulishwa uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Kariobangi Sharks
Aidha kwa wapinzani wa Yanga, wametakiwa kujiandaa 'kisaikolojia' kwani hawataamini watakachokiona..!
"Sasa tunatambua katika wiki ya kufunga kazi na kukusanya vijiji, miji na majiji, wapo watakaopigwa na bumbuwazi, wapo watakaopata hofu kubwa kutokana na silaha kali za Yanga tutakazozitambulisha kwenye kilele cha wiki ya mwananchi"
"Pia wapo wapinzani watakaopoteana kwa sababu hawaamini wanachokiona"
"Kwa watakaopatwa na hayo, tunaomba radhi lakini hakuna namna!"
"Sisi Daima mbele, nyuma mwiko. Wiki nzima ni shughuli za kijamii, kisha August 4 ni kilele ambapo tutacheza na Kariobangi Sharks Uwanja wa Taifa"