Uongozi wa Yanga umelipongeza tawi la Nguvu ba Buku kwa kukarabati Wodi ya Wagonjwa Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam
Jana viongozi wa Tawi hilo walikamilisha ukarabati wa Wodi ya Wanaume ambao uligharimu karibu Milioni mbili
"Ni uandishi wa historia mpya katika soka la nchi yetu, ni uwekaji wa alama zitakazodumu milele kuonyesha kwamba Yanga ni timu ya wananchi kweli," imesema taarifa ya Yanga
"Hongera sana Tawi la Nguvu ya Buku (Mwanayamala) kwa kukarabati wodi ya wanaume katika hospitali ya eneo lenu kama inavyoonekana"
"Tunatambua jitihada kubwa zinazofanywa na Wanayanga nchini kote katika kuhakikisha wiki ya Mwananchi inakuwa na tija kwa Taifa letu"
ADVERTISE HERE