Leo Jumanne asubuhi kikosi cha Yanga kitajipima dhidi ya Friends Rangers ukiwa ni mchezo wa kirafiki
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema mchezo huo una lengo la kukipima kikosi chake, ukiwa ni mchezo wa pili ambao ataushuhudia tangu arejee nchini
Zahera amesema kikosi kitakachoanza mchezo huo hakitahusisha wachezaji waliocheza mchezo dhidi ya Mawenzi Market juzi
Mcongomani huyo anaendelea na maandalizi ya kikosi chake mkoani Morogoro wakitarajiwa kurejea jijini Dar es salaam siku ya Ijumaa
ADVERTISE HERE