Serikali Zanzibar yaunga mkono Yanga, yaahidi kusaidia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Jul 2019
Serikali Zanzibar yaunga mkono Yanga, yaahidi kusaidia

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi ameunga mkono mfumo wa klabu ya Yanga kuanzisha miradi ya kujitegemea katika azma ya kuiondoshea na utegemezi.

Balozi Seif Ali Iddi ameyasema hayo ofisini kwake Vuga-Zanzibar wakati akizungumza na Uongozi wa Yanga uliowakilishwa na Mwenyekiti Dk Mshondo Msolla

Balozi Seif amesema kwa kuwa Klabu hiyo ina dhamira sahihi ya kuendeleza Wachezaji wake katika azma njema ya kuimarisha ustawi wao, yeye binafsi pamoja na Serikali iko tayari kusaidia nguvu zake ili kuona malengo iliyojipangia yanafanikiwa vizuri.

Mwenyekiti wa Yanga Dr. Mshindo Msolla amemueleza Balozi Seif kwamba uongozi umelenga kuyasimamia mambo matano makubwa yatakayosaidia kuipeleka klabu hiyo katika mafanikio.

Mambo hayo ni pamoja na kuleta umoja katika kuipeleka timu kwa wanachama, kuimarisha Miradi iliyopo klabuni na kubuni mengine mipya, uwajibikaji na utawala bora pamoja na kuiendeleza miradi iliyopo Visiwani Zanzibar.

Amesema katika mfumo huo Mpya utakaoanzishwa, Wanachama watakuwa na uwezo wa kujua mapato na matumizi ya klabu kupitia mtandao wa kisasa wa Habari na Mawasiliano utakaokwenda sambamba na kuongeza Wanachama kutoka 17,000 hadi kufikia Milioni 1,000,000.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
3m ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
15h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
18h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
23h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’