Klabu ya Yanga kwa kushirikiana na kampuni ya GSM, leo wametambulisha jezi za timu hiyo zitakazotumika msimu wa 2019/20 katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam
Akizungumza katika utambulisho wa jezi hizo, Mwakilishi wa GSM ambao ndio waliotengeneza na wasambazaji, amesema hakuna jezi yenye ubora zaidi ya jezi za Yanga hapa Tanzania
Tayari jezi hizo zinapatikana kwenye maduka ya GSM Msasani Mall, Pugu Mall na makao makuu ya Yanga
"Hakuna jezi yenye ubora kama huu nchini Tanzania. Pia tutafungua duka kubwa la vifaa mbalimbali vyenye nembo ya Yanga, hamjawahi kuona duka la Kimataifa kama hilo"

Nae Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema hii ni nafasi kwa mashabiki wa Yanga kuichangia timu yao kwa kununua jezi halisi ambazo zimezinduliwa rasmi leo
"Wakati nazunguka kwenye matawi ya Yanga mashabiki na wanachama walikua wananiambia hawataki kununua jezi kwa sababu club hainufaiki"
"Sasa nawambia wanunue kwa sababu club inanufaika"
Msimu ujao Yanga itakuwa jezi za aina mbili, kijani kwa ajili ya nyumbani na njano kwa ajili ya ugenini

