Uongozi wa klabu ya Yanga umewataka mashabiki wake kufurika uwanja wa Taifa kuianza safari ya Kimataifa leo
Saa 12 jioni, Yanga itashuka 'kwa Mkapa' kuumana na Township Rollers kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa hatua ya awali
"Safari ya Kimataifa imeshaanza dude linaamka leo pale uwanja wa Taifa, Township Rollers wanaenda kukaa"
"Tanzania ni nchi yenye Umoja na Mshikamano, hivyo hatutaruhusu kirahisi timu yetu yoyote ya nyumbani ipoteze pointi tatu dhidi ya timu ya nje"
"Tutasapoti Taifa Letu na Timu zetu zote za Tanzania zinazoshiriki mashindano ya CAF"
"Ajabu itakua wewe Mwananchi na Mzalendo kubaki nyumbani"
Uzuri bei ni za wananchi, viingilio kwa Mzunguko ni Tsh 5,000 VIP B na C Tsh 15,000 tu. Na VIP utakaa kwa Tshs. 50,000 tu
Tayari mashabiki wameanza kusogea uwanja wa Taifa kuelekea mchezo huo ambao utaanza saa 12 jioni